Maswali yatawasaidia viongozi kutadhimini na kupima jinsi huduma inavyoendelea juu ya uanafunzi. Majibu ya maswali haya yatadhihirisha kama kuandaa wanafunzi ni kipaumbele na kama utaratibu/mkakati wa kuandaa wao unafanyiwa kazi na mikakati ya iliyowazi kwa waamini.
Rasilimali za lugha ya uanafunzi
Video za Mafunzo
rasilimali za pdf
Uanafunzi unaobeba maono na mikakati
Muhtasari huu umeandikwa kwa madhumuni ya kusaidia kanisa la Kikristo kupata maono wazi ya ni nini, na jinsi ya, kuwafunza watoto wa Mungu kwa vipaumbele, zana, na mikakati.Ni matumaini kuwa utapata taarifa inayoweza kukusaidia katika kuandaa uanafunzi ndani ya kanisa lako.
Msingi wa kweli wa Mkristo
Zawadi kuu tuliopokea kupitia wokovu ni uwezo wa kuwa karibu na kutengeza uhusiano wa kipekee na Mungu.Uanafunzi ni mkakati mahususi wa Mungu kujifunza namna ya kuwa kama Kristo. Na namna ya kuishi katika maisha ya kumtukuza yeye(Mungu).Vitabu vya ibada ya KIMUNGU inathihirisha umuhimu wa kweli wa kibibilia juu ya imani ya Kikristo inayopaswa kwa waamini wote kujifunza.Yesu Kristo ni mwamba wetu Tunakaa ndani yake lakini ikiwa msingi mtu kiroho ni dhaifu huathiri moja kwa moja maisha yake.Hizi pia ni nyenzo au silaha kwa wale waliofanyika wanafunzi Au kuwafundisha wengine kuwa wanafunzi.
Ndoa ni huduma
Mfululizo wa ndoa ni huduma imegawanyika katika juzuu tano vinachimbua makusudi ya Mungu juu ya ndoa, huanisha majukumu ya mume na mke, hufunua au huweka wazi baraka ambazo Mungu alikusudia katika ndoa,Na kutoa mifano mahususi juu ya namna wanandoa wanavyopaswa kuhudumiana wao kwa wao.Mfumo hufanya kazi kuu kwa wanandoa wapya,Katika kuwa na msingi na ndoa imara, nyezo za ushauri , kuwafanya wengine au vikundi vidogo kuwa wanafunzi.
Malezi ni huduma
Mfululuzo wa malezi ni huduma inakupa juzuu nne yenye kuchimbua kusudio la Mungu katika wajibu wa mzazi kupenda , kulea na kuwafunza watoto katika njia iwapasayo kuenenda.Hii hulenga kusaidia wazazi/walezi wasio na mfano mzuri.na huwasidia kutoa kanuni za kibibilia na ukweli unaofunua makusudi ya Mungu juu ya malezi.mfumo hutoa kanuni ya wazi ya namna kuwalea watoto hadi kuwa watu wazima.
Msamaha na upatanisho
Kijitabu hiki chenye ukarasa 14 hutambulisha kanuni za kibibilia juu ya msamaha na hatua za kupatinisha uhusiano ulioharibika. Ni nzuri na hupendekezwa kama nyezo binafsi za kujinzia au kama nyenzo ya ushauri.